Godfrey Mushi, Arusha.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Fedha na Uchumi kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kilichoketi leo kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha ushirikiano wa Jumuiya hiyo pamoja na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/2024, Kikao hicho kimeketi katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Jijini Arusha.
Washiriki wengine kutoka Tanzania walikuwa ni Waziri wa Viwanda na Biashara , Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba, Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Gavana wa
Benk Kuu , Bw. Emmanuel Tutuba, Kamishna Mkuu wa TRA , Bw. Alphayo Kidata, Kamishna wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Elijah Mwandumbya na Maafisa waandamizi wa Serikali kutoka Wizara kadhaa nchini na Mataifa mengine ya Afrika Mashariki.
Dkt Nchemba ameongoza jopo la wataalamu kutoka Tanzania katika kuhakikisha maslahi ya nchi yetu yanawekwa mbele kwa manufaa ya maendeleo ya Wananchi.
Facebook Comments