Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba1 (Mb), tarehe 9 Juni, 2023, amepokea jumla ya gawio la Shilingi bilioni 45.8 kutoka Benki ya @CRDBBankPlc , ikiwa ni gawio kwa Serikali Kuu, Taasisi na Mashirika yake kutokana na uwekezaji ndani ya Benki hiyo.

Mwaka huu Benki ya CRDB imetoa jumla ya gawio la Shilingi bilioni 117.5 kwa Wanahisa wake baada ya kupata faida ya shilingi bilioni 351.4 baada ya kodi mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko la 31% ikilinganishwa na faida ya shilingi bilioni 268.2, mwaka 2021.

Share Story

Facebook Comments