Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo June 17,2023 amekuwa Mgeni rasmi kwenye halfa ya kukabidhi gawio na sherehe za miaka 25 ya Benki ya NMB Mlimani City Jijini Dar es salaam ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kuipongeza NMB @NMBTanzania kwa kuiweka Tanzania kwenye ramani ya Kimataifa kwakuwa ni Benki ya tatu kwa faida katika Sekta ya Kibenki ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Nashukuru kwa kunipa mwaliko na sikuweza kukataa kwakuwa najua nakuja kupokea fedha ndefu kwa ajili ya Serikali, tunaipongeza Benki ya NMB, kuna tafiti inasema Taasisi yenye Menejmenti inayoanza na Wanawake watatu hiyo Menejiment inakuwa vizuri na ni tafiti iliyofanywa Tanzania kuhusu Mashirika ya Umma kwahiyo hii Bodi inafanya vizuri kwasababu Menejimenti ina Wanawake, Mtendaji Mkuu Mwanamke ingawa Bodi Wanaume watupu na ni meseji yangu Bodi ijayo Wanawake tuwemo”
“Hatuwezi kuwa na Taifa linalojitegemea kama Wananchi wake ni tegemezi, kujenga Taifa linalojitegemea hutokana na uwezeshwaji wa Wananchi hususani Wajasiriamali wadogo na wa kati jambo ambalo NMB mmejitahidi kulifanya kwa nafasi yenu, tunaadhimisha miaka 25 ya safari ndefu ya mafanikio ya NMB ikiwa ni Benki Kiongozi nchini katika kutengeneza faida na sasa imeiweka Nchi yetu kwenye ramani ya Kimataifa kwakuwa ni Benki ya tatu kwa faida katika Sekta ya Kibenki ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye Nchi saba sasa hivi”
“Vilevile NMB imekuwa Benki ya kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara na hati fungani maalum inayomlenga Mwanamke maarufu kama Jasiri Gender Bond hiyo ndio imetupa sifa kabisa kabisa kabisa, nawashukuru kwa kuja na wazo hili ni wazo zuri ambalo linaibeba safari yangu ya Uchampion kwa suala la Generation Equality, hii inakwenda kunibeba vizuri na utakuwa mfano wangu mzuri sana”
Nae Dkt Mwigulu Nchemba akimkaribisha Rais Samia Suluhu Hassan amesema
“Benki ya NMB ni Benki ambayo imeweka Mizizi kwenye nchi yetu na imeunganika na wanachi wetu moja kwa moja
Leo NMB kuweza kutoa gawio la Bilioni 45 ambalo ni kubwa zaidi katika historia ya taasisi za kifedha hapa nchini ni uthibitisho wa namna sekta binafsi imezidi kuimarika chini ya uongozi wako Mheshimiwa Rais.
Facebook Comments