Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiongoza kikao cha kujadili taarifa ya utekelezaji wa ukusanyaji mapato ya ndani ya Serikali ya mwaka 2023/24, ambapo Serikali inatarajia kukusanya kodi ya ndani, shilingi trilioni 26.72, kwa upande wa Tanzania Bara na shilingi bilioni 520.64 kwa upande wa Zanzibar, ambapo ili kuwezesha kukusanya kwa ufanisi zaidi mapato hayo, Serikali imefanya maboresho mbalimbali kwenye masuala ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Kikao hicho kimewashirikisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Salum Mkuya, Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu-TAMISEMI, Bw. Adolf Ndunguru, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya,  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Lucy Kabyemera Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Alphayo Kidata, Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA), Bw.   Yusuph Mwenda, Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Hazina Ndogo jijini Dar es Salaam.

Share Story

Facebook Comments