Serikali imesema hesabu zinazowasilishwa na CAG kila mwaka ni uhakika.
Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba, ametoa kauli hiyo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Konde, Mohammed Said Issa aliyetaka kujua kama hesabu zinazowasilishwa na CAG kila mwaka ni za mashaka au uhakika.
“Mheshimiwa Spika, hesabu zinazowasilishwa na maafisa masuuli kwa CAG kila mwaka ni za uhakika kwa kuwa zinaandaliwa na kuwasilishwa kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 30 (2) cha Sheria ya Fedha za Umma, SURA 348;
“Viwango vya kimataifa vya uhasibu katika sekta ya umma (IPSAS); miongozo mbalimbali inayotolewa na Wizara ya Fedha; na mifumo madhubuti ya kielektroniki ya usimamizi wa fedha ikijumuisha mfumo wa uhasibu serikalini (MUSE).
“Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita (2019/20 – 2021/22), taarifa ya CAG imeonesha ongezeko la hati zinazoridhisha kutoka asilimia 92 mpaka 96 kwa serikali kuu; asilimia 70 mpaka 94 kwa serikali za mitaa; na kupungua kutoka asilimia 97 mpaka 98 kwa mashirika na taasisi nyingine za umma,” amesema Waziri Nchemba.
Kwa upande mwingine Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa wanalishughulikia suala la mabadiliko ya bei ya Dola ili kukabiliana jambo hilo la upungu wa Dola ambalo kwa sasa linasumbua ulimwengu kwa ujumla.
Dkt. Mwigulua ameyasema hayo leo Agosti 29, 2023 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge Jimbo la Mbogwe Mhe. Nicodemas Maganga aliyetaka kujua Serikali inampango gani wa kudhibiti mabadiliko ya bei ya Dola.
Katika majibu yake Dkt. Mwigulu amesema kuwa tatizo hilo la upungufu wa Dola linasababisha mahitaji ya Dola kuwa makubwa kuliko upatikanaji wake na kupelekea bei yake kubadilikabadilaka
Aidha Dkt. Mwigulu amesema kuwa Kuna hatua ambazo wamezichukua ambazo zitasaidia Dola ziwe nyingi sokoni ili kupunguza bei ya Sasa ya Dola.
Facebook Comments