Leo tumemkabidhi mkandarasi wa Kampuni ya Henan Highway Engineering Group Limited ya China mradi wa ujenzi wa barabara ya Sabasaba – Sepuka – Ndago hadi Kizaga, kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 77.6.

Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupatia fedha nyingi za miradi ya maendeleo, tunamshukuru kwa kuwezesha ujenzi wa barabara hii ya kimkakati ambayo inaenda kufungua lango la uchumi kwa wanachi wa mkoa wa singida, Barabara hii inakwenda kurahisisha na kuharakisha shuguli za biashara, kilimo na huduma za usafiri.

Nawashukuru waheshimiwa Mawaziri Mheshimiwa Innocent Bashungwa kwa kukubali kuja kukabidhi mradi huu kwa mkandarasi, namshukuru kaka yangu Mheshimiwa Waziri Profesa Kitila Mkumbo kwa kukubali kuja kushiriki nasi katika shuguli hii. Kipekee pia niwashukuru Viongozi wa dini kwa kuendelea kushirikiana nasi katika shuguli za maendeleo na kuendelea kuliombea Taifa Amani, Maendeleo na Mshikamano.

Nawashukuru waheshimiwa wabunge wote walioshirikiana nasi siku ya leo wakiwemo, Elibariki Kingu, Yahya Masare, Dkt Chaya, Martha Gwau, Aisharose Matembe, madiwani, wananchi wote wa Jimbo la Iramba Magharibi, Singida Magharibi na watumishi wote wa umma.

Share Story

Facebook Comments