“Alipoingia Dkt. Samia alielekeza kuondoa usumbufu huu ambao Wananchi wanaupata na akamuelekeza Gavana wa Benki kuu na Idara inayosimamia Microfinance ndani ya Wizara ya Fedha kupitia upya masharti ya utoaji wa leseni hizo ambazo Watu wanatumia vibaya na kuweka riba wanajipangia nyingine mara 50%, mara 100% nyingine mara 200% na si hawa Wananchi wa kawaida tu hata Watumishi wa Umma wenyewe wapo kwenye kilio hiki”

“Kinachofanyika sasa hivi leseni zote zimepitiwa upya na zinatolewa kwa masharti kama ambavyo mabenki yanayotoa kwahiyo hakutokuwepo na huo uholela ambao Mtu alikuwa anaamka tu anajiamulia anafanya hivyo na pia hivi tunavyoongea kuna leseni zimeshafutwa kwasababu ya masharti hayo ya riba kubwa ambazo hazina ubinadamu ndani yake na pia kwasababu ya unyanyasaji”

“Kuna baadhi ya kausha damu wana Mahabusu zao, Mtu akifika hapo wanamweka Mahabusu yao ambayo ni kinyume cha taratibu waliofanya hivyo leseni tayari zimeshafutwa, kwahiyo kama kuna jambo mahususi linaendelea iwe Singida au eneo lolote Wananchi wafike ofisi ya Mkuu wa Mkoa waandikishe, tutatuma Timu yetu itaenda itachukua hatua na tukijiridhisha tutafuta leseni hizo”

Share Story

Facebook Comments