Serikali ya Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimesaini mikataba miwili yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 158.1 (sawa na shilingi za Tanzania, bilioni 398.7) kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Kimataifa wa Reli ya Kisasa (SGR) utakaoziunganisha nchi ya Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), pamoja na kuiongezea mtaji Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB).

Mikataba hiyo imesainiwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), kwa niaba ya Serikali na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Patricia Laverley, katika Ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo Jijini Dar es Salaam, na kushuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bw. Emmanuely Lyimo na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.

Share Story

Facebook Comments