Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kuendeleza sekta ya ujenzi ili sekta hiyo iweze kuongeza mchango wake katika Uchumi na maendeleo ya watu. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri wa Fedha, jijini Dodoma.
Mkutano huo uliwashirikisha pia Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Mhandisi Godfrey Kasekenya, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mhe. Balozi Mhandisi Aisha Amour na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara hizo.
Facebook Comments