Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb), jijini Dodoma, ambapo walijadili masuala ya maendeleo ya sekta ya elimu ikiwemo kuanza kwa matumizi ya mtalaa mpya wa masomo nchini.

 

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Dkt. Franklin Rwezimula na Mkurugenzi wa Mipango Bw. Atupele Mwambene (katikati) pamoja na Viongozi wengine waandamizi kutoka Wizara hizo mbili.

Share Story

Facebook Comments