Waziri wa Fedha na Mbunge Jimbo la Iramba Magharibi mkoani Singida, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amefanya mikutano ya hadhara na wananchi wa Kata za Ntwike, Mgongo na Shelui katika TARAFA ya Shelui Wilayani Iramba, mkoani Singida.

Akiongea na wananchi hao kwa nyakati tofauti Mhe. Dkt. Nchemba amewahakikishia kuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atajenga barabara za kisasa na zenye ubora wa hali ya juu nchi nzima ili kukomesha kabisa kuharibika kwa barabara na kukatika kwa mawasiliano yanayotokea kipindi cha mvua.

Mhe. Dkt. Nchemba amesema Dkt Samia Suluhu Hassan, anataka uchumi wa Wananchi uweze kukua kwa kasi hivyo ni lazima miundombinu hiyo iwe imara ili iweze kupitika kipindi chote cha mwaka mzima.

Wakati huohuo amesema katika kupindi cha miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, Serikali imefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa nchini ikiwemo Jimbo la Iramba Magharibi katika Sekta za Elimu, Afya, Umeme, Barabara n.k, nankutoa wito kwa wananchi waendelee kuiamini Serikali kwani Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuhakikisha wananchi wake wanabadilisha hali zao kiuchumi na kijamii.

Dkt Nchemba anaendelea na ziara yake Wilayani humo kwa kusikiliza na kutatua changamoto na kupokea maoni ya wananchi kuelekea kwenye Bunge la Bajeti linalotarajia kuanza wiki ijayo jijini Dodoma.

Share Story

Facebook Comments