Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kufungua uchumi wa Wananchi kwa kuwajengea mazingira rafiki ya uzalishaji na usafirishaji watanzania.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha (Mb) Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba akiwa kwenye maadhimisho ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Singida yaliyofanyika Kata ya Sepuka Wilayani Ikungi tarehe 06 Aprili, 2024.
“Mhe. Rais amefanya mambo makubwa sana kwa muda mfupi, ametoa ruzuku kwenye Mbolea ili iwe nusu bei, ameongeza bajeti kila sekta, ikiwemo ya Barabara, umeme, Maji, Kilimo ambapo kila kijiji kimeguswa na miradi mingi tunaiona, lakini pia amejenga Vituo vya Afya, Elimu bure mpaka kidato cha sita na Elimu ya Kati wanapata mikopo kama ilivyo Elimu ya juu” Alisema Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba.
‘’Dunia nzima inampa heshima kubwa Rais wetu kwasababu alipokea nchi wakati mgumu,Taifa likiwa msibani, Uviko 19 ukiwa umeua uchumi wa dunia, mgogoro wa Urusi na Ukraine ukiwa umeshamiri lakini Mhe Rais alipambana na vyote hivyo na kutuvusha Salama’’ amesema Dkt Nchemba.
Dkt Nchemba alimaliza kwa kuwapongeza Jumuiya ya Wazazi kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya na amewatia moyo waendelee kumsaidia Mhe Rais na Mwenyekiti wa CCM Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Facebook Comments