Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amewasili Washington D.C nchini Marekani ambapo ameongoza ujumbe wa Tanzania unaohudhuria Mikutano ya majira ya kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) yenye kaulimbiu ya “Vision to Impact”.
Akiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alipokea Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ubalozi kutoka kwa Mhe. Balozi Dkt. Elisie Kanza, ambapo amempongeza Balozi na timu yake kwa kazi kubwa ya kuiwakilisha nchi na kusimamia kikamilifu na kwa umahili masuala ya diplomasia ya uchumi ambapo amemwahidi ushirikiano.
Mkutano huo uliwashirikisha Viongozi mbaoimbali wakiwemo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba na Viongozi wengine wa Wizara, Idara na Taasisi zake.
Facebook Comments