Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameshiriki Mkutano wa Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) katika Nchi za Afrika Kundi la Kwanza (Africa Group I Constituency – IMF) chini ya uenyekiti wa Waziri wa Fedha wa Namibia, Mhe. Lipumbu Shiimi, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) yenye kauli mbiu ya “Vision to Impact” inayoendelea jijini Washington D.C, nchini Marekani. Katika Mkutano huo Magavana walipokea ripoti ya mpito ya shughuli za utendaji kazi wa AfG1 kwa kipindi cha kuanzia Oktoba 2023 hadi Aprili 2024.
Ripoti hiyo imeainisha makubaliano ya nchi wanachama kutaka Taasisi za Fedha za Kimataifa (Benki ya Dunia na IMF) kuongeza viwango vya ufadhili ili nchi hizo ziweze kutekeleza miradi ya maendeleo katika nchi zao, kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi, kukabiliana na njaa na kukuza teknolojia zitakazo saidia kuongeza ajira na masuala mazima ya uwekezaji.
Facebook Comments