Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Msaidizi wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye pia ni Mkurugenzi wa Afrika wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Ahunna Eziakonwa, ambapo wamejadiliana masuala ya ushirikiano kati ya Tanzanis na Shirika hilo hususan mpango utakao iwezesha nchi kupata mikopo yenye gharama (riba) nafuu zaidi katika masoko ya fedha ya kimataifa. Mkutano huo umefanyika Katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, kando ya Mkutano ya kipupwe inayoendelea Jijini Washington D.C nchini Marekani.
Facebook Comments