Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) ameitaka Benki ya Dunia kubadili Sera yake ya Manunuzi kwa kupunguza masharti magumu yanayowabana Makandarasi wazawa kupata Miradi mikubwa.

Dkt Mwigulu Nchemba (almarufu Mr Clean) alisema hata kama Fedha hizo ni za Mkopo,bado ni Fedha za Watanzania kwa kuwa madeni hayo yatalipwa na watanzania. Na Uwepo wa sheria inayofanya makampuni ya kigeni yawe na sifa zaidi za kupata miradi na wazawa kushindwa kwa kukosa dhamana ni kuifanya Nchi yetu kuwa bomba la kupitishia fedha na kwenda mataifa mengine na sisi kubaki na Mzigo wa madeni.

Akijibu hoja ya Mr Clean, Makamu wa Rais wa Benki hiyo anayesimamia MIGA, Ndugu Junaid Kamal Ahmad, alisema Dkt Mwigulu Nchemba ameeeleza kwa uzalendo mkubwa sana masuala ya Nchi ya Tanzania, na hana shaka na uzalendo wake kwani hata tai yake inamtambulisha wazi, na amekubaliana na hoja yake, watakaa na watalaam warekebishe utaratibu huo kwajili ya Maslahi ya wananchi wa Tanzania.

Share Story

Facebook Comments