Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) amesema hawezi kuvumilia kuona maskini wanaendelea kutozwa kodi kwenye biashara ndogondogo ilihali kuna matajiri wameshindwa kesi katika Mahakama za Kodi na hawajalipa kodi wanazodaiwa Kama ilivyoamriwa katika mashauri yao.

Dkt Nchemba amesema kuendelea kuwatoza maskini kodi ni kuwafanya waendelee kuwa maskini zaidi ilihali kuna Matrillion hayajakusanywa kutokana na uzembe.

“Kodi ni Tool ya Kuondoa Pengo ya Walionacho na Wasionacho, We have to Tax the Rich and give Services to the Poor . Sisi tukiwapa ahueni Matajiri alafu tukawatoza Maskini, tutawawafanya Masikini Waendelee kuwa Masikini “ – alisema Dkt. @mwigulunchemba

Ameyasema hayo wakati akifanya kikao kazi na Mamlaka ya Mapato (TRA), Bodi ya rufani za kodi (TRAB ) na Baraza la rufani za kodi (TRAT)

Share Story

Facebook Comments