Kutafuta na kukusanya mapato ya shilingi trilioni 44.19, kati ya maoteo yote ya Serikali ya kukusanya jumla ya shilingi trilioni 49. 35 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya Serikali;

· Kuimarisha na kusimamia mifumo ya mapato, matumizi na mali za Serikali ikiwemo IDRAS, TANCIS, MUSE, NeST, CBMS na GAMIS;

· Kuhudumia deni la Serikali kwa wakati na kuboresha kanzidata ya kutunza taarifa za deni;

· Kutoa elimu ya huduma za fedha kwa wananchi kwa lengo la kukuza huduma jumuishi za fedha nchini; na

· Kujenga uwezo kwa wakaguzi wa ndani, kamati za ukaguzi pamoja na waratibu wa usimamizi wa vihatarishi katika taasisi za umma.

Share Story

Facebook Comments