Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) anawasilisha Hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali, ambapo ameliomba Bunge, kwa mwaka 2024/25, Serikali ridhaa ya kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 49.35, sawa na ongezeko la asilimia 11.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/24.

Ongezeko la bajeti kwa kiasi kikubwa limetokana na kugharamia: deni la Serikali ambalo limeongezeka kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi, kuongezeka kwa viwango vya riba na kuiva kwa mikopo ya zamani; ajira mpya; ulipaji wa hati za madai; Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024; maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025; na maandalizi ya michuano ya mpira wa miguu ya mataifa ya Afrika (AFCON) ya mwaka 2027, ikiwemo ujenzi na ukarabati wa viwanja.

Share Story

Facebook Comments