Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Bw. Yusuf Mwenda, Katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha Jijini Dar es salaam, ambapo wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha utendaji kazi wa Taasisi hiyo muhimu huku jambo kubwa likiwa ni kuweka mikakati ya kutekeleza maelekezo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili kuboresha ukusanyaji kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Share Story

Facebook Comments