Waziri wa Fedha, Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ametoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa ili liendelee kuwa na umoja wa kitaifa ulioletwa na falsafa za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Dkt. Nchemba ametoa rai hiyo wakati akiwahutubia waumini wa Kanisa la Kikatoliki Jimbo la Geita, alipohudhuria Jubilei ya Miaka 25 ya upadre ya Askofu Flavian Matindi Kassala, yaliyofanyika Kanisa Kuu Bikira Maria Malkia wa Amani, Mkoani Geita.

“Ni vyema kutambua kwamba tunahitaji kushindanisha sera na falsafa zinazolenga kuendeleza na kuunganisha Taifa letu na sio kuleta mgawanyiko na kubaguana”

Aidha, Dkt Nchemba amewaomba viongozi wa dini kuendelea kushirikiana na Serikali kutoa elimu na kukemea masuala ya ukatili wa watoto na kijinsia yanayofanywa katika jamii.

Share Story

Facebook Comments