Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba Lameck Madelu (Mb), ameungana na abiria wengine kutumia usafiri wa treni ya mwendo kasi (SGR), kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na kuonja ladha ya usafiri huo ambao Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa mradi huo wa kimkakati unafika nchini kote na kuchangia kuchochea biashara katika ukanda wa Maziwa Makuu. Aliyekaa pembeni yake ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Mhandisi Ismail Hassan Rumatila.
Facebook Comments