Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na walimu wake waliomfundisha katika Shule ya Sekondari Ilboru iliyopo Mkoani Arusha.

Walimu hao ambao wengi ni wastaafu waliambatana na walimu waliopo sasa wa shule hiyo. Mhe. Dkt. Nchemba alifanya nao mazungumzo baada ya ziara yao ya kutembelea Bunge, jijini Dodoma, ambapo amewashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa ya kuwafundisha wanafunzi ambao mchango wao umekuwa mkubwa katika ujenzi wa Taifa.

 

Share Story

Facebook Comments