Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa, amefunga rasmi Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma la Nchi za Afrika, Jijini Arusha na kuzishauri nchi hizo za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia Mifumo wa Ununuzi ya Kidijitali katika nchi zao kama ilivyo kwa Tanzania, ambayo imezindua Mfumo wake wa Ununuzi wa NeST, ambao lengo lake ni kuongeza ufanisi na uwazi katika Sekta ya Ununuzi.
Facebook Comments