Mkuu wa Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Mhe. Mheshimiwa Johari Samizi, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuipatia Wilaya yake, zaidi ya shilingi bilioni 39 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ambazo zimeelekezwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo sekta za afya, elimu, maji na mingine mingi.

Mhe. Samizi, ametoa shukrani hizo wakati alitoa salaam za Wilaya na Mkoa wa Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Said Mtanda, wakati wa Mapokezi ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), aliyeanza ziara ya kikazi ya siku 7 mkoani Mwanza ambapo anatarajia kutembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi ya maendeleo katika Wilaya zote za mkoa wa Mwanza.

Share Story

Facebook Comments