Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ameshiriki mjadala kuhusu umuhimu wa matumizi ya Nishati safi ya kupikia, akimwakilisha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa Taasisi ya Africa50 (General Shareholders Meeting – GSM) na Jukwaa la Miundombinu la Afrika (Infra for Africa Forum meeting) Taasisi ambayo Tanzania ni mwanachama, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Ivato, Mjini Antananarivo, nchini Madagascar.
Facebook Comments