Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) amehutubia mamia ya wananchi wa Misungwi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Amani, Misungwi Mjini, ambapo alitoa wito kwa Watanzania na watu wote wenye mapenzi mema na nchi yetu, kuendelea kumwombea kwa Mwenyezi Mungu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili awe na afya njema anapotekeleza majukumu yake ya kuwahudumia watanzania kwa upendo na ari kubwa.

Alisema Serikali imeendelea kutoa fedha nyingi wakati huu kuliko wakati wowote ule ambapo kila mahali nchini, inatekelezwa miradi ya maendeleo inayogharimu fedha nyingi, ikiwemo miradi ya kimkakati kama SGR, umeme wa Bwawa la Julius Nyerere, Ujenzi wa Daraja la Kigongo-Busisi na mingine mingi katika sekta za uzalishaji, afya, maji, elimu, miundombinu nk

Share Story

Facebook Comments