Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amewasili Washington D.C nchini Marekani, ambapo ameongoza ujumbe wa Tanzania unaohudhuria Mikutano ya Mwaka (Annual Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF), yenye kaulimbiu ya “Vision to Impact”.
Akiwa katika Ubalozi wa Tanzania, Mhe. Dkt. Nchemba alipokea Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya ubalozi kutoka kwa Mhe. Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza, ambapo amempongeza Balozi na timu yake kwa kazi kubwa ya kuiwakilisha nchi.
Ujumbe wa Tanzania umewahusisha Viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Nd. Aboud Hassan Mwinyi, Gavana wa Banki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, anayesimamia Sera za Fedha na Uchumi Dkt. Yamungu Kayandabila, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mcha Hassan Mcha na Viongozi wengine waandimizi wa Serikali.
Facebook Comments